Ninawezaje kuleta bot langu la uuzaji kwenye Deriv Bot?
Vuta faili la XML kutoka kwenye kompyuta yako hadi eneo la kazi, na bot lako litapakiwa kulingana na hilo. Vinginevyo, unaweza kubofya Import kwenye Bot Builder, na uchague kuleta bot lako kutoka kwenye kompyuta yako au Google Drive.
Kuleta kutoka kwenye kompyuta yako
- Baada ya kubofya Import, chagua Local kisha ubofye Continue.
- Chagua faili lako la XML kisha ubofye Open.
- Bot lako litapakiwa kulingana na hilo.
Kuleta kutoka kwenye Google Drive yako
- Baada ya kubofya Import, chagua Google Drive kisha ubofye Continue.
- Chagua faili lako la XML kisha ubofye Select.
- Bot lako litapakiwa kulingana na hilo.






