
Kupanda na kushuka kwa soko la hisa ni sehemu ya kawaida ya mchezo huu. Siku nyingine bei hupanda kama roketi, na siku nyingine hushuka kwa kasi kuliko roller coaster. Ikiwa unafanya biashara, kuelewa kuyumba kwa bei ni muhimu ili ufanye maamuzi bora na ubaki na udhibiti wa mkakati wako.
Mwongozo huu unaeleza kuyumba kwa bei katika soko la hisa ni nini, kwa nini hutokea, na jinsi unavyoweza kukabiliana nako kama mtaalamu.
Hisa ni nini? (muhtasari mfupi!)
Hisa (zinazoitwa pia equities) zinawakilisha umiliki katika kampuni. Unaponunua hisa, unakuwa mwanahisa, yaani unamiliki sehemu ya kampuni hiyo. Kampuni ikifanya vizuri, thamani ya hisa zake kwa kawaida hupanda, na ikiwa inakabiliwa na changamoto, bei ya hisa inaweza kushuka. Wafanyabiashara hununua hisa wakitarajia kupata faida kutokana na kupanda kwa bei na gawio (ambalo ni sehemu ya faida ya kampuni inayogawiwa kwa wanahisa).
Kwa nini bei za hisa hubadilika-badilika?
Soko la hisa hufanya kazi kwa msingi wa ugavi na mahitaji. Watu wengi wakitaka kununua hisa kuliko kuuza, bei hupanda. Watu wengi wakitaka kuuza kuliko kununua, bei hushuka. Inaonekana rahisi, lakini kwa uhalisia bei huathiriwa na mambo mengi, ikiwa ni pamoja na hali ya uchumi, hisia za wafanyabiashara, na hata habari za dharura.
Kuyumba kwa bei katika soko la hisa ni nini?
Kuyumba kwa bei hupima kiasi ambacho bei za hisa hupanda na kushuka. Bei zikibadilika kwa kasi na kwa kiwango kikubwa, soko linakuwa tete sana. Zikienda kwa utulivu, kuyumba kwa bei ni kwa kiwango cha chini. Ni muhimu kutambua kwamba kuyumba kwa bei hakukuambii iwapo bei zitapanda au zitashuka. Kunapima tu ukubwa wa mienendo ya bei.
Mfano halisi:
Katika siku za mwanzo za janga la COVID-19, soko la hisa lilishuhudia mabadiliko makubwa ya kila siku kwa sababu hakuna aliyejua nini kingefuata. Kutokuwa na uhakika = kuyumba zaidi kwa bei.
Aina mbili za kuyumba kwa bei:
- Kuyumba kwa bei kwa kihistoria: Hupima kiasi ambacho bei ya mali imebadilika huko nyuma. Kuangalia mienendo ya bei ya zamani huwasaidia wafanyabiashara kukadiria mabadiliko yanayoweza kutokea baadaye.
- Kuyumba kwa bei kunakodokezwa: Huonyesha kiasi ambacho wafanyabiashara wanatarajia hisa kubadilika siku zijazo. Mara nyingi hupatikana kutokana na bei za chaguo na ni muhimu katika kutabiri mabadiliko yanayoweza kutokea ya bei.
Jinsi ya kupima kuyumba kwa bei
Wafanyabiashara hutumia zana mbalimbali kupima kuyumba kwa bei katika soko la hisa:
- Beta: Unyeti wa hisa ukilinganishwa na fahirisi ya marejeleo (k.m., S&P 500). Beta iliyo juu ya 1 inamaanisha hisa hiyo inayumba zaidi kuliko fahirisi, huku beta iliyo chini ya 1 ikimaanisha ina utulivu zaidi.

- VIX (Fahirisi ya Kuyumba kwa Bei): Pia huitwa “kipimo cha hofu,” VIX hupima kuyumba kwa soko kunakotarajiwa katika siku 30 zijazo. VIX inayopanda kwa kawaida huashiria kutokuwa na uhakika na uwezekano wa mabadiliko makubwa ya bei. VIX hukokotolewa na Chicago Board Options Exchange (CBOE).
Nini husababisha kuyumba kwa bei katika soko la hisa?
Mambo kadhaa huchangia kuyumba kwa bei katika soko la hisa, yakiwemo:
Mambo ya uchumi mkuu (Picha kubwa)
- Mishtuko ya kiuchumi: Migogoro ya kimataifa, mdororo wa uchumi, au mabadiliko ya sera yanaweza kutikisa soko.
- Sera ya fedha: Wakati benki kuu zinapopandisha au kushusha viwango vya riba, huathiri imani ya soko.
- Matukio ya kisiasa: Uchaguzi, vita vya kibiashara, na migogoro ya kijiografia na kisiasa vinaweza kuleta kutokuwa na uhakika na mabadiliko makubwa ya soko.
Mambo ya uchumi mdogo (Yanayohusu kampuni mahususi)
- Ripoti za mapato: Kampuni ikizidi matarajio ya mapato, bei ya hisa zake mara nyingi hupanda ghafla. Isipofikia matarajio, tarajia kushuka.
- Mienendo ya sekta: Mabadiliko katika teknolojia, kanuni, au tabia za watumiaji yanaweza kuathiri sekta nzima.
- Habari za kampuni: Mkurugenzi Mtendaji kujiuzulu au ununuzi mkubwa wa kampuni vinaweza kusababisha mabadiliko makubwa ya hisa.
Jinsi ya kukabiliana na kuyumba kwa bei katika soko la hisa
Kuyumba kwa bei si jambo baya kila wakati. Baadhi ya wafanyabiashara hunufaika nako. Lakini ni muhimu kuwa na mpango. Hii hapa ni mikakati ya kukusaidia kukabiliana na mabadiliko ya soko:
- Tofautisha biashara zako: Sambaza biashara zako katika sekta mbalimbali ili kupunguza hatari.
- Fikiria muda mrefu: Zingatia ukuaji wa muda mrefu, si kelele za muda mfupi za soko.
- Tumia dollar-cost averaging: Fanya biashara kwa kiasi kisichobadilika mara kwa mara, bila kujali kinachoendelea sokoni.
- Rekebisha jalada lako la biashara: Rekebisha biashara zako mara kwa mara ili kudumisha kiwango cha hatari unachopendelea.
- Endelea kupata taarifa: Fuatilia habari za kiuchumi na mwenendo wa masoko ili kutarajia kuyumba kwa bei kunakoweza kutokea.
Kuyumba kwa bei katika soko la hisa si jambo la kuogopa. Ni jambo la kuelewa na kudhibiti. Iwe wewe ni mfanyabiashara wa siku moja unayetafuta mabadiliko ya haraka au mfanyabiashara wa muda mrefu unayevuka misukosuko ya soko, kuwa na mikakati sahihi kutakufanya ujiamini katika hali yoyote ya soko.
Uko tayari kujaribu mikakati yako katika masoko tete? Jisajili kwa akaunti ya demo ya Deriv bila malipo yenye pesa za kidijitali za USD 10,000 na ujaribu ujuzi wako wa biashara leo!
Quiz
Ni kipi kati ya yafuatayo SIO sababu ya kuyumba kwa soko la hisa?


