
Udhibiti wa hatari ni siri ya mafanikio ya muda mrefu katika uuzaji udhibiti wa hatari. Bila huo, hata mikakati bora inaweza kuporomoka. Hapo ndipo kiashiria cha Average True Range (ATR) viashiria vya kiufundi kinapoingia. Ni kipimo cha kuaminika cha tete ya soko, kinachokusaidia kukabiliana na mabadiliko ya bei kwa kujiamini.
Average True Range (ATR) ni nini?
Fikiria ATR kama kigunduzi cha hali ya soko. Kiashiria hiki, kilichobuniwa na J. Welles Wilder Jr., hakitabiri mwelekeo wa bei. Kinapima tu kiasi ambacho mali husogea, iwe ni hisa, sarafu, bidhaa, au fahirisha toleo. Mienendo mingi zaidi? ATR ya juu zaidi. Soko tulivu? ATR ya chini zaidi. Rahisi, sivyo? Hujirekebisha kulingana na hali tofauti za soko, na hivyo kuwa zana nzuri ya udhibiti wa hatari.
Kwa nini wafanyabiashara hupenda ATR
Wafanyabiashara hutumia ATR hasa kwa sababu mbili kuu:
- Kuamua ukubwa wa nafasi: ATR hukusaidia kurekebisha ukubwa wa biashara yako kulingana na jinsi soko lilivyo tete. Tete zaidi? Punguza ukubwa wa nafasi yako kwenye masoko tete. Katika hali tulivu zaidi, unaweza kuzingatia kuuongeza kidogo.
- Viwango vya Stop Loss na Take Profit vya busara: ATR hukusaidia kuepuka kutolewa kwenye biashara mapema mno kwa kuweka malengo halisi ya bei yanayolingana na mabadiliko ya soko.
Jinsi ya kutumia ATR kwenye majukwaa ya uuzaji ya Deriv
Habari njema! Huhitaji kufanya hesabu mwenyewe. Majukwaa ya CFD ya Deriv hukokotoa ATR kiotomatiki kwa ajili yako. Iongeze kwenye chati yako ili uanze kuitumia kwenye mkakati wako wa hatari.
Ikiwa una hamu ya kujua hesabu iliyo nyuma yake, ATR hupatikana kwa kuchukua thamani kubwa zaidi kati ya:
- Kiwango cha juu cha sasa kukitoa kiwango cha chini cha sasa
- Thamani kamili ya kiwango cha juu cha sasa ukitoa bei ya kufunga ya awali
- Thamani kamili ya kiwango cha chini cha sasa ukitoa bei ya kufunga ya awali
Kisha, hupatiwa wastani katika kipindi kilichowekwa (kwa kawaida siku 14). Kipindi kirefu zaidi hulainisha mstari lakini huchelewa kuitikia mabadiliko ya ghafla.

Kutumia ATR kwa udhibiti wa hatari
Kuweka Stop Loss na Take Profit kama mtaalamu
ATR hukusaidia kuweka viwango vya Stop Loss na Take Profit kwa busara zaidi. Ikiwa ATR ya Volatility 25 Index ni USD 8.5 na kiingilio chako ni USD 100:
- Unaweza kuweka Stop Loss yako kwa mara 2 ya ATR (USD 83)
- Na Take Profit yako kwa mara 3 ya ATR (USD 125.50)
Tete inapokuwa juu, kuweka viwango vya Stop Loss na malengo mbali zaidi kunaipa biashara yako nafasi zaidi ya kupumua.
Kuamua ukubwa wa nafasi kwa urahisi
ATR pia ni nzuri kwa kuamua biashara yako inapaswa kuwa kubwa kiasi gani. Kanuni ya kawaida? Hatarisha kipimo 1 tu cha ATR kwa kila biashara. Hivyo, ikiwa ATR ni USD 8.5, utahatarisha upeo wa USD 8.5 kwenye biashara hiyo. Hii huweka hatari yako chini ya udhibiti huku ikiendana na mienendo ya asili ya soko.
Mambo machache ya kukumbuka
ATR ni muhimu, lakini kama kiashiria chochote, ina mapungufu. Hii ndiyo sababu:
- Ni kiashiria kinachochelewa: ATR huangalia mienendo ya bei ya zamani, kwa hivyo haitabiri siku zijazo, bali hukusaidia kujiandaa kwa ajili yake.
- Hutumika vyema pamoja na zana nyingine: Hakuna kiashiria kimoja kinachoweza kufanya kila kitu. Changanya ATR na uchambuzi wa kiufundi na wa kimsingi kwa maamuzi bora ya uuzaji.
ATR ni kama msaidizi mwaminifu katika udhibiti wa hatari. Haitabiri siku zijazo, lakini itakupa tahadhari thabiti kuhusu hali ya soko. Kabla ya kuitumia kwenye biashara halisi, jizoeze kutumia ATR kwenye akaunti ya demo ya Deriv ili uone jinsi inavyounga mkono maamuzi yako ya uuzaji.
Uko tayari kufanya biashara kwa kujiamini zaidi?
Quiz
Ikiwa thamani ya ATR itapanda ghafla, hilo linamaanisha nini?


