
Uuzaji wa crypto umekuwa ukipata kasi kwa miaka mingi, ukiwapa wafanyabiashara urahisi, usalama na fursa za kusisimua. Lakini kwa wale ambao bado hawajaanza, imani potofu zinaweza kufanya ionekane ngumu au isiyoweza kufikiwa. Hebu tuweke mambo wazi na kuvunja hadithi potofu tatu za kawaida kuhusu kufanya biashara kwa crypto!
Hadithi potofu ya 1: Kumiliki crypto ni gharama kubwa
Sivyo kabisa! Ingawa bei ya Bitcoin inaweza kuonekana ya kutisha, si lazima ununue Bitcoin nzima ili kuanza. Unaweza kumiliki sehemu ndogo sana zake zinazoitwa satoshis. Kwa mfano, kwenye Deriv, kiasi cha chini cha biashara kwa Bitcoin ni 0.0001 BTC tu, ambacho kwa sasa kina thamani ya chini ya USD 5!
Zaidi ya hayo, kuna njia nyingine ya kufanya biashara ya crypto bila gharama kubwa ya awali: uuzaji wa leverage kwa CFDs. Njia hii hukuruhusu kufungua nafasi kubwa zaidi kwa mtaji mdogo wa kuanzia, hivyo kufanya biashara ya crypto ipatikane kwa urahisi zaidi kuliko unavyodhani.
Hadithi potofu ya 2: Utahitaji kujifunza soko jipya kabisa
Unadhani crypto ni ulimwengu tofauti kabisa? Si lazima! Ikiwa tayari unajua jinsi ya kufanya biashara ya forex, hisa au masoko mengine, crypto ni aina nyingine tu ya mali unayoweza kuongeza kwenye mkakati wako.
Mchakato unafanana: Chagua soko lako, chagua aina ya biashara, na udhibiti hatari yako. Unaweza hata kutumia sarafu za crypto kufanya biashara kwenye masoko mengine kama forex au fahirisi za synthetic. Kwa hiyo, hujifunzi mchezo mpya kabisa. Unaongeza tu zana nyingine kwenye mkakati wako wa biashara.
Hadithi potofu ya 3: Njia pekee ya kupata crypto zaidi ni kuinunua
Kununua crypto ni njia moja tu ya kuimiliki, lakini si njia pekee. Unapofanya biashara kwa sarafu ya crypto kwenye masoko kama forex au synthetics na kupata malipo, unaongeza salio lako la crypto.
Ni kama kupata kipato kwa sarafu ya kawaida. Tofauti ni kwamba safari hii faida yako iko katika crypto. Kwa kufanya biashara kwa busara, unaweza kukuza umiliki wako wa crypto bila kufanya manunuzi ya ziada.
Gundua uuzaji wa crypto kwa akaunti ya demo ya Deriv ya bure
Sarafu za crypto zinabadilisha jinsi tunavyofanya biashara, zikitoa fursa mpya zaidi ya sarafu za kawaida za jadi. Kwa kuelewa ukweli nyuma ya hadithi hizi potofu, unaweza kugundua uuzaji wa crypto kwa kujiamini na kwa mtazamo mpya.
Angalia aina zote za sarafu za crypto zinazopatikana kwa biashara kwenye Deriv, na ufungue akaunti ya biashara ya mazoezi bila malipo leo!
Quiz
Kipimo kidogo zaidi cha Bitcoin kinaitwaje?


