Hati hii ni sehemu ya makubaliano kati yako na Deriv na inapaswa kusomwa pamoja na Masharti ya Jumla ya Matumizi kwa wateja ("Masharti ya Jumla"). Maneno yoyote yaliyofafanuliwa yanayotumika katika masharti haya ya ziada yatakuwa na maana iliyotolewa kwao katika Masharti ya Jumla.
1. Utangulizi
1.1. Masharti haya ya ziada yanawahusu wateja wote walio na akaunti na Deriv Investment Bank (Labuan) Ltd.
1.2. Iwapo kutakuwa na kutofautiana au mikengeuko kati ya masharti haya ya ziada na/au hati nyingine yoyote inayounda sehemu ya Makubaliano, masharti haya ya ziada yatashinda kuhusiana na akaunti yako na Deriv Investment Bank (Labuan) Ltd.
1.3. Deriv Investment Bank (Labuan) Ltd. imepewa leseni chini ya Labuan Financial Services and Securities Act kufanya biashara ya kusimamia fedha (money-broking) kutoka au kupitia Federal Territory of Labuan, Malaysia, na inaidhinishwa na kudhibitiwa na Labuan Financial Services Authority.
2. Utekelezaji wa maagizo
2.1. Kwa kuzingatia sharti la leseni yetu, tunatenda kama wakala kwa niaba yako pale tunapotekeleza maagizo yako, na sisi si mshirika wa upande wa pili katika biashara zako.
2.2. Wakati agizo linapowekwa kununua au kuuza chombo cha kifedha (instrument) kwenye akaunti yako ya Deriv MT5, agizo lako hupitishwa kwa mtoa huduma wa ukwasi (liquidity provider) anayetupatia huduma. Hatushiriki katika kuchukua nafasi yoyote (position taking) kwenye biashara zako.
2.3. Tunahitajika kufanya uchunguzi wa kina (due diligence) kwa watoa huduma wote wa ukwasi na kuhakikisha kuwa mahali tunapotumia (venues) yanadhibitiwa na mamlaka inayotambulika ya usimamizi au udhibiti.