Je, kamisheni inahesabiwaje kwa biashara zinazofanyika kwenye Deriv cTrader?
Kwa kila mteja mpya unayemwelekeza ambaye anakamilisha biashara yake ya kwanza kwenye Deriv kati ya tarehe 15 Aprili na 30 Mei 2026, unapata dola 3 za ziada juu ya gawio lako la kawaida. Hakuna kiwango cha chini kinachohitajika — kila biashara ya kwanza inahesabiwa.
Kamisheni = (Kiasi cha biashara kwa USD) × (Kiwango cha kamisheni) ÷ 100,000
Kukokotoa kiasi cha biashara kwa USD:
Kiasi cha biashara kwa USD = (Kiasi kwa lot) × (Ukubwa wa kontrakt) × (Bei ya utekelezaji) × (Kiwango cha ubadilishaji kwenda USD)
Mfano wa hesabu kwa kutumia BTC/USD
Tuseme:
- Umefanya biashara ya lot 1 ya BTC/USD
- Kila kontrakt = Bitcoin 1
- Bei ya sasa ni USD 60,000
- Kiwango cha ubadilishaji = 1 (kwa kuwa ni katika USD)
- Kiwango cha kamisheni (upande mmoja) ni USD 10 kwa kila USD 100,000 zinazofanyiwa biashara
Jinsi ya kukokotoa:
1. Tafuta kiasi cha biashara kwa USD:
1 (lot) × 1 (ukubwa wa kontrakt) × 60,000 (bei) × 1 (kiwango cha USD) = USD 60,000
Hivyo, jumla ya kiasi cha biashara = USD 60,000
2. Tumia fomula ya kamisheni:
Kamisheni = (60,000 × 10) ÷ 100,000 = USD 6
Hivyo, kamisheni ya USD 6 kwa upande mmoja
3. Ikiwa utafungua na kufunga biashara (round trade):
6×2 = 12
Jumla ya kamisheni ya USD 12