
Bidhaa ni malighafi zinazoendesha ulimwengu, kuanzia kahawa iliyo kikombeni mwako hadi dhahabu iliyo kwenye vito vyako. Zimekuwa zikifanyiwa biashara kwa karne nyingi, tangu enzi za Njia ya Hariri, na leo bado ni sehemu kubwa ya uchumi wa dunia. Kimsingi, bei za bidhaa hutegemea kanuni moja rahisi: ugavi na mahitaji.
Mahitaji yanapokuwa makubwa na ugavi ukiwa mdogo, bei hupanda sana. Kinyume chake kikitokea, bei hushuka. Ni rahisi hivyo tu!
Aina mbili za bidhaa
| Bidhaa ngumu | Bidhaa laini | ||
|---|---|---|---|
| Metali | Nishati | Kilimo | Mifugo na nyama |
| Dhahabu | Mafuta ghafi | Soya | Ng'ombe hai |
| Fedha | Gesi asilia | Kahawa | Nguruwe wasio na mafuta mengi |
| Shaba | Petroli | Nafaka | Maziwa |
| Platinamu | Pamba | ||
Bidhaa ziko katika aina kuu mbili:
- Bidhaa ngumu. Hizi ni rasilimali asilia zinazochimbwa au kutolewa ardhini, kama mafuta, dhahabu na metali.
- Bidhaa laini. Hizi ni pamoja na mazao ya kilimo kama ngano, kahawa na sukari.
Baadhi ya bidhaa maarufu zaidi katika ulimwengu wa biashara ni mafuta (hasa WTI na Brent crude) na dhahabu, ambayo imekuwa chaguo la wafanyabiashara kila uchumi unapoonekana kuyumba.
Jinsi ya kuboresha ujuzi wako wa biashara ya bidhaa
Unataka kuboresha ujuzi wako wa biashara ya bidhaa? Hizi hapa ni hatua chache muhimu:
- Elewa kinachosababisha bei kubadilika
Mwenendo wa kiuchumi, matukio ya kisiasa na hata majanga ya asili vinaweza kutikisa bei za bidhaa. Kwa mfano, dhoruba kubwa inaweza kutatiza uzalishaji wa mafuta na kusababisha bei kupanda kwa kasi. Kufuatilia habari za dunia kunaweza kukupa faida zaidi.
- Tumia uchambuzi wa soko
Wafanyabiashara hutegemea aina kuu mbili za uchambuzi:- Uchambuzi wa msingi (kuangalia ugavi, mahitaji na hali ya kiuchumi)
- Uchambuzi wa kiufundi (kutumia data ya bei za kihistoria kutambua mifumo)
- Fuata mwenendo
Bidhaa husogea kwa mwenendo, ama juu (bullish) au chini (bearish). Kutambua mwenendo huu mapema kunaweza kukusaidia kufanya biashara kwa wakati unaofaa.
Jinsi ya kufanya biashara ya bidhaa kwenye Deriv
Huhitaji kumiliki mapipa ya mafuta au vipande vya dhahabu ili kufanya biashara ya bidhaa. Badala yake, unaweza kufanya biashara hiyo kwa kutumia CFDs (Contracts for Difference) au Chaguo kwenye Deriv. Hivi ndivyo:
Biashara ya CFD kwenye Deriv
Fanya biashara ya bidhaa kwenye majukwaa kama Deriv MT5, Deriv cTrader na Deriv X ukitumia CFDs, ambayo hukuruhusu:
- Kuchukua nafasi ya long (kununua) ikiwa unadhani bei zitapanda.
- Kuchukua nafasi ya short (kuuza) ikiwa unatarajia bei zitashuka.
Nafasi yako hubaki wazi kwa muda wowote upendao, hivyo kukupa udhibiti zaidi wa mkakati wako wa biashara.
Biashara ya Chaguo kwenye Deriv
Ikiwa unapendelea hatari iliyopangwa, jaribu chaguo za kidijitali kwenye metali ukitumia mikataba ya Rise/Fall, Higher/Lower au Touch/No Touch. Mikataba hii hukuruhusu kutabiri mabadiliko ya bei ndani ya muda uliowekwa.
- Rise/Fall. Tabiri ikiwa bei itaishia juu au chini kuliko ilipokuwa ulipoingia.
- Higher/Lower. Weka bei lengwa (barrier) na utabiri ikiwa soko litamalizia juu au chini yake.
- Touch/No Touch. Tabiri ikiwa soko litafikia bei maalum.
Ukiwa na Chaguo, utajua faida au hasara yako inayowezekana kabla ya kuingia kwenye biashara, jambo linalofanya usimamizi wa hatari kuwa rahisi zaidi.
Uko tayari kuanza kufanya biashara ya bidhaa?
Biashara ya bidhaa inasisimua kwa sababu bei hubadilika kutokana na matukio halisi duniani, hivyo kutoa fursa na hatari pia. Siri ya mafanikio? Endelea kujifunza, kuwa mwepesi kubadilika, na fanya biashara kwa busara.
- Fanya mazoezi ukitumia akaunti ya demo ya Deriv ili kujenga kujiamini! Utapata USD 10,000 za fedha pepe za kufanya mazoezi kabla ya kuingia kwenye biashara halisi.
- Jisajili leo na uanze kuchunguza soko la bidhaa!
Quiz
Ni bidhaa gani mara nyingi hujulikana kama “dhahabu nyeusi”?


