75% ya akaunti za wawekezaji wa rejareja hupoteza pesa wanapofanya biashara ya CFDs na Deriv. Unapaswa kuzingatia ikiwa unaweza kumudu kuchukua hatari kubwa ya kupoteza pesa zako.

CFD ni vyombo tata vyenye hatari kubwa ya kupoteza pesa haraka kutokana na leverage. 75% ya akaunti za wawekezaji wa rejareja hupoteza pesa wanapofanya biashara ya CFDs na mtoa huduma huyu. Unapaswa kuzingatia ikiwa unaelewa jinsi bidhaa hizi zinavyofanya kazi na ikiwa unaweza kumudu kuchukua hatari kubwa ya kupoteza pesa zako.

Ninawezaje kutambua barua pepe kutoka kwa matapeli wanaojifanya ni watu wa msaada kwa wateja toka Deriv?

Hapa kuna baadhi ya njia za kutambua barua pepe kutoka kwa matapeli:

  • Barua pepe imeandikwa vibaya, ina makosa ya kisarufi, na makosa mengi ya tahajia.
  • Matapeli watakwambia utume taarifa za siri kupitia majukwaa yasiyo salama, kwa mfano, kupitia SMS, WhatsApp, barua pepe, n.k.
  • Wanakwambia ujaze fomu kwenye wavuti isiyosalama bila unganisho la HTTPS (salama).
  • Wanakwambia upakue apps za simu zisizo salama katika mfumo wa APK faili ambazo hazitolewi kwenye Google play store au App Store.
  • Wanakwambia upakuze viambatisho vya faili au programu za upatikanaji wa mbali (kama Teamviewer) kuwapa udhibiti wa mbali wa kifaa chako. Kwa mfano, tapeli anayeiga anaweza kuchukua udhibiti na kusakinisha programu hatarishi ya ransomware kwenye kifaa chako kisha kudai fidia. Ikiwa fidia haitalipwa, huenda ukapoteza kabisa uwezo wa kufikia kifaa chako.
  • Matapeli mara nyingi hutumia vikoa vya barua pepe bila malipo kama @yahoo.com, @gmail.com, au @protonmail.com. Daima soma anwani kamili ya barua pepe ya mtumaji ili kujua ni nani aliyetuma barua pepe hiyo. Kumbuka: Barua pepe kutoka Deriv zitakuja kila mara kutoka @deriv.com.