Ninawezaje kuwatambua matapeli wanaojifanya ni watu wa msaada kwa wateja toka Deriv kwenye Telegram?

Lengo kuu la tapeli ni kuiba taarifa zako muhimu na fedha zako.
Hizi ni baadhi ya njia za kutambua wajifanyao kuwa huduma kwa wateja wa Deriv:
- Wajifanyao wanauliza maelezo yako ya kuingia au taarifa nyingine nyeti kupitia Telegram.
- Wanatoa zawadi zinazoonekana kuwa nzuri mno hivi kwamba haziwezi kuwa za kweli.
- Wanadai malipo kupitia njia zisizoweza kufuatiliwa, kwa mfano, kupitia cryptocurrency.
- Wanakwambia upakue app ambayo haijatolewa kwenye Google Play Store au Apple App Store.
- Wanakwambia upakue programu inayoruhusu kifaa chako kudhibitiwa kwa mbali.
- Wanakwambia upakue faili zenye programu hasidi au virusi vinavyoweza kuathiri kifaa chako.
Bila shaka, orodha hii haijakamilika. Kila siku, matapeli wanakuja na mbinu mpya kujaribu kuiba taarifa zako na pesa.









