Kanuni zetu

Tumepewa heshima kubwa kumhudumia kila mtu anaetegemea bidhaa na huduma zetu, na tunataka tu kutoa kilicho bora zaidi. Ndio sababu kanuni zetu na maadili ni muhimu sana katika kufafanua sisi ni nani, kwa nini tunafanya kile tunachofanya, na jinsi tunavyowashughulikia wateja wetu na watu wengine. Katika ofisi zetu mbalimbali za kimataifa, tumejitolea kufata kanuni zifuatazo katika kila kitu tunachofanya.

Kuwa mwaminifu

Mikataba yote inakamilishwa kwa haki, usahihi, na kwa uharaka

Tutaweka bei na kukamilisha mikataba yote kwa usahihi na kwa haki, kulingana na data za kuaminika zinazotolewa na bila ucheleweshwaji, ili wateja waweze kuamini bei zetu kwenye wavuti.

Kushughulikia uwekaji na utoaji wote wa pesa haraka na kwa usahihi

Tutaunda mifumo yetu ya keshia ili kufanya kazi kwa usawa iwezekanavyo, kushughulikia uwekaji na utoaji kwa ufanisi na haraka. Kwa kadiri iwezekanavyo, tutapunguza ucheleweshwaji uliowekwa na AML au mahitaji yoyote ya kupambana na ulaghai.

Kutoa biashara ya mtandaoni inayoaminika ikiwa na muda wa kutosha, usalama mzuri, na usumbufu kidogo.

Tunalenga kuwapa wateja wetu mifumo ya kuaminika ambayo ina muda wa juu wa matumizi na muda mchache wa kusubiri, hata kwenye mitandao ya simu yenye kasi ndogo ya data. Tunatoa usalama mzuri na utangamano wa vifaa vikuu vyote katika desktop na simu.

Kutoa msaada kwa mteja wenye manufaa kwa wateja wote

Tutajitahidi kutoa huduma ya mazungumzo mubashara 24/7 ili kufanya mawakala kupatikana kwa ajili ya mteja yoyote anayeomba mazungumzo. Mawakala watafunzwa kujibu maswali husika kuhusu huduma.

Kuwa mwadilifu

Wateja wote huudumiwa kwa usawa

Tutawahudumia wateja wote kwa usawa, bila kujali wanatoka wapi au ukubwa wa akaunti zao.

Kushughulikia malalamiko yote kwa uadilifu

Katika tukio la malalamiko yoyote, tunalenga kutatua suala hilo kwa kasi na uadilifu.

Kutoa bei za ushindani kwenye bidhaa zetu zote

Tunakusudia kuwa na ushindani juu ya bei kwa bidhaa na huduma zetu zote.

Hakuna gharama iliyofichwa

Tutakuwa wazi juu ya ada na makato yote.

Hakuna vizuizi bandia katika utoaji pesa kwa wateja

Ikiwa mteja ana haki ya ushindi au salio, na hakuna wasiwasi wa ulaghai au mahitaji ya AML, wanapaswa kuwa na uwezo wa kutoa fedha hizo wakihitaji.

Kuwa wazi

Ongea tu kirahisi na kwa uwazi, wala usijifiche nyuma ya utata

Tutatumia lugha nyepesi katika bidhaa zetu zote, huduma, na mawasiliano.

Kufunua masharti ya mikataba yote

Tutakuwa wazi juu ya masharti ya mikataba yote ili wateja waweze kufanya uchaguzi sahihi.

Kufunua kwa uwazi na kwa uelewea hatari zinazohusiana na biashara

Tutakuwa wawazi juu ya hatari zote zinazohusiana na biashara kwa sababu tunataka wateja wetu wafanye chaguzi wakiwa na taarifa kulingana na hamu yao ya hatari.

Kufichua jinsi tunavyopata pesa

Tutakuwa wazi kuhusu jinsi tunavyopata pesa, ikiwa ni pamoja na wakati sisi ni washirika wa biashara au tunafanya kazi kama broker.

Kutoa uwakilishi wa uzoefu na demo

Uzoefu wa biashara na demo utaakisi uhalisia wa biashara halisi ya pesa, haswa katika mikataba ya bei na vikwazo vya kibiashara.

Kuwa mwajibikaji

Hakuna ugumu katika kuuza

Tutakuwa waaminifu katika utangazaji wetu. Hatutatumia picha zisizofaa za mafanikio ya kifedha katika nyezo zetu za masoko.

Hakuna ushauri wa kifedha au kibiashara

Hatutatoa maoni yoyote juu ya mwelekeo wa soko au ufanisi wa biashara yoyote mahususi.

Hakuna ahadi za hakikisho la faida

Hatutasema kuwa biashara inatatua wasiwasi wa mtu wa kifedha au inaweza kuzalisha mapato ya kuaminika. Tutakuwa wazi kuwa hakuna faida za uhakika au zisizo na hatari katika biashara.

Kutekeleza sera za kuzuia watu walio hatarini kufanya biashara

Tutawanyima watu wenye umri mdogo ufikiaji na kushughulikia utekelezaji wa kutambua wateja wanaofanya biashara zaidi ya uwezo wao wa kifedha.

Kutekeleza udhibiti ili kuzuia shughuli zilizo kinyume na sheria

Tutatekeleza udhibiti wa mjue mteja wako (KYC) na kuzuia utakatishaji wa pesa na shughuli zingine zilizo kinyume na sheria kwenye majukwaa yetu.